Deuteronomy 4:1-6

Waamriwa Utii

1 aSikia sasa, ee Israeli, amri na sheria nitakazokufundisha wewe. Zifuate ili upate kuishi na uingie kuimiliki nchi ambayo Bwana, Mungu wa baba zako anawapa. 2 bUsiongeze wala usipunguze chochote ninachowaamuru ninyi, ila myashike maagizo ya Bwana Mwenyezi Mungu wenu ambayo nawapa.

3 cMliona kwa macho yenu wenyewe kile Bwana alichokifanya kule Baal-Peori. Bwana Mwenyezi Mungu wenu aliwaangamiza kutoka miongoni mwenu kila mmoja aliyemfuata Baali wa Peori, 4lakini ninyi nyote mlioshikamana na Bwana kwa uthabiti, Mungu wenu, mko hai mpaka leo.

5 dTazama, nimewafundisha amri na sheria kama Bwana Mwenyezi Mungu wangu alivyoniamuru mimi, ili mzifuate katika nchi mnayoiingia kuimiliki. 6 eZishikeni kwa uangalifu, kwa kuwa hii itaonyesha hekima na ufahamu wenu kwa mataifa, ambayo yatasikia kuhusu amri zote hizi, nao watasema, “Hakika taifa hili kubwa ni watu wenye hekima na ufahamu.”
Copyright information for SwhKC